Hyppää sisältöön
Yksinäinen mänty Harriniemen hiekkarannalla. Etualalla vaaleanpunaisia kasveja.

Kiswahili

 • Njia rahisi – Kwa sehemu kubwa njia ina miti mirefu. Njia rahisi kwa kiasi.

  Njia inayohitaji bidii isiyokuwa na kizuizi – upana wa miti mirefu mpaka mnara wa ndege wa Rummelö ni sentimeta 100, ambapo baada yake miti mirefu inapungua. Kutoka njia panda ya mnara wa ndege wa Rummelö inawezekana kuendelea bila kizuizi kupitia Harrinniementie kwenda kwenye mnara wa taa.

  Njia ya asili ya Rummelö- Harrbådan inapita kwenye msitu mzuri kwenye uwanda ulioinuka karibu na bahari. Njia inapindapinda kwenye mitete na misitu ya pwani. Kondoo wanaokula majani kwenye eneo hilo wanatunza mazingira na kuwafurahisha wanaotembea hapo kipindi cha joto. Harrinniemi kuna mnara wa taa wa jengo la sementi la zamani, ambao inasemwa kuwa una mizimu. Njia inaishia kwenye pwani yenye mchanga kwenye ncha ya rasi karibu na bahari.

  Kipindi cha barafu njia ya asili haishughulikiwi, lakini iko wazi kutumiwa na wanaotembea. Hapo karibu kuna mtandao mkubwa wa njia na kwa wanaotembea kuna njia za kipindi cha barafu, ambazo zinashughulikiwa pia wakati wa kipindi cha barafu. Kipindi cha barafu njia ya kuteleza kwenye theluji ni kwa ajili ya wanaocheza mchezo wa kuteleza kwenye theluji.

  Usitembee kwenye maeneo yanayozunguka nyumba binafsi za shambani. Sehemu zingine za eneo la Harrinniemi ziko huru kwa matumizi ya wote. Ili kutunza uasili unaoharibika haraka tembea kwa kufuata sehemu zilizowekewa alama kwenye njia.

  • Unapotembea weka umakini muda wa kutaga kwa ndege 15.4.–31.7.
  • Tunafuata kanuni za kutokuchafua wakati wa kutembea.
  • Wakati wa tahadhari ya moto wa msituni hairuhusiwi kuwasha moto.

  Njia ya kuteleza kwenye theluji

  Njia ya kuteleza kwenye theluji yenye taa

  Njia ya kuteleza kwenye theluji iliyo kwenye barafu

  Njia ya asili

  Njia ya nje

  Njia isiyokuwa na kizuizi

  Njia ya baiskeli

  Njia ya mtumbwi

  Njia ya kipindi cha barafu

  Eneo la Natura 2000

  Uko hapa

 • Njia inayohitaji bidii isiyokuwa na kizuizi – Njia ni pana iliyotengenezwa kwa changarawe.

  Njia ya kutembea ya Trullevi inapita kwa kiasi kwenye eneo la hifadhi ya Taifa ya bustani ya mji wa Kokkola. Njia inayozunguka mazingira ya msitu inakwenda mara zote kutoka mjini mpaka kwenye ncha ya rasi.

  Sehemu ya thamani zaidi ya eneo hilo la asili ni shamba la shetani na makonde ya bahari na maziwa ya flada (linalotengenezwa na bahari) yaliyotengenezwa na muinuko wa ardhi. Ziwa la kluuvi (linalotengenezwa na bahari) Nisulanpotti ni sehemu inayopendwa na ndege kutaga mayai (kuweka viota). Wanyama wengi wanafurahia Trullevi, kama sili, kuchakuro wanaoruka na nungunungu.

  • Kipindi cha barafu kufuatana na hali ya theluji njia hii inakuwa njia ya kuteleza kwenye theluji, na wakati huo hairuhusiwi kwa wengine kutembea kwenye njia hii.
  • Kutoka kwenye njia hii unaweza kuendelea mpaka kwenye uwanja (rinki) wa barafu. Weka umakini kwenye usalama unapotumia uwanja wa barafu. Usiende kwenye barafu ambayo haijaganda vizuri.
  • Unapotembea weka umakini muda wa kutaga kwa ndege 15.4.–31.7.
  • Tunafuata kanuni za kutokuchafua wakati wa kutembea.
  • Wakati wa tahadhari ya moto wa msituni hairuhusiwi kuwasha moto.

  Njia ya kuteleza kwenye theluji

  Njia ya kuteleza kwenye theluji yenye taa

  Njia ya kuteleza kwenye theluji iliyo kwenye barafu

  Njia ya asili

  Njia ya nje

  Njia isiyokuwa na kizuizi

  Njia ya baiskeli

  Njia ya mtumbwi

  Njia ya kipindi cha barafu

  Eneo la Natura 2000

  Uko hapa

  • Heshimu hali ya uasilia.
  • Fuata njia zilizowekewa alama.
  • Weka umakini kwa wengine wanaotembea kwenye hali ya asili.
  • Hakikisha uwezekano wa kuwepo kwa mipaka ya kutembea kwenye sehemu unayotembea.
  • Mfunge mnyama unayemfuga kwa mkanda wake.
  • Fuata kanuni za kutokuchafua wakati wa kutembea.

  Inaruhusiwa

  • kutembea kwa miguu, kuteleza kwenye theluji au kwa baiskeli sehemu zingine mbali na kwenye maeneo ya nyumba na maeneo yaliyowekwa kwa matumizi maalum, kama mashamba yanayotumika kwa kilimo na maeneo
  • ya kuoteshea miche kwa muda mfupi, ambako pia inaruhusiwa kutembea, kwa mfano kuweka hema kwenye umbali unaotosha kutoka kwenye makazi
  • kuchuma matunda ya porini, uyoga na maua
  • kuvua samaki kwa ndoano na kwa kuchimba kwenye barafu
  • kutembea kwenye maji na kwenye barafu.

  Hairuhusiwi

  • kusababisha usumbufu au madhara kwa wengine au mazingira
  • kusumbua ndege wanaotaga na wanyama wengine
  • kukata au kuharibu miti
  • kuchukua kuvumwani, kuvu, mboji au kuni
  • kusumbua amani ya nyumbani
  • kuchafua
  • kuendesha chombo cha moto kwenye eneo la ardhi ya mtu bila ruhusa ya mmiliki wa ardhi
  • kuvua samaki au kuwinda bila ruhusa ya mhusika.
 • Kwenye njia ya kutembea ya Kokkola tunafuata kanuni za kutokuchafua wakati wa kutembea. Hii inamaanisha kuwa, anayetembea asiache hata mabaki yake kwenye eneo la asili. Kutembea bila kuchafua kunatunza mazingira na kwa kupitia hiyo itakuwa vizuri kutembea kwenye hali ya asili hata siku zijazo.

  Takataka zinazoachwa kwenye asili inasababisha hatari kwa wanyama na mazingira. Takataka zinazoingia kwenye maji ni hatari kwa viumbe vya kwenye maji na pia kwenye mfumo wa ekolojia. ndio sababu tunachukua takataka zote pamoja nasi tunapotoka kwenye hali ya asili na maeneo ya kutembea.

  Kwa pamoja tutunze mazingira yetu!

  Kanuni za kutokuchafua wakati wa kutembea

  • Anayetembea asiache mabaki yake kwenye eneo la asili. Wakati unapoondoka punguza kiwango cha uchafu.
  • Tumia vifaa vya kufungashia vya kudumu, vinavyoweza kutumika upya.
  • Peleka uchafu wa vyakula yaani uchafu unaooza kwenye choo cha samadi kilichopo sehemu ya mapumziko au kwenye mashine ya kutengeneza samadi. Usiweke uchafu wa vyakula kwenye vyombo vya kukusanya uchafu mchanganyiko.
  • Unaweza kutumia kiasi kidogo cha karatasi safi na maboksi kwa kuwashia moto mahali pa kuwashia moto au kwenye mafiga yaliyo kwenye kibanda cha kupikia. Hairuhusiwi kuchoma moto uchafu mwingine, kwa sababu unaweza kutengeneza hewa yenye sumu na uchafu ambao hauwezi kuharibiwa.
  • Chukua uchafu wa hatari na uchafu mchanganyiko kutoka kwenye ardhi ya eneo hilo.
  • Wakati wote safisha uchafu wako na ikihitajika pia uchafu wa wengine. Ni vizuri kuwa na kiasi kidogo cha mifuko ya plastiki kwa ajili ya kukusanya uchafu unaoonekana kwenye ardhi ya eneo hilo.
  • Kusanya vichungi vya sigara kwenye vyombo vyako mwenyewe na utupe uchafu huo baadaye kwenye sehemu ya kutupa uchafu.

  Piirros, jossa Kokko-Lokki kantaa roskapussia kivisessä maastossa reppu selässään.

  Kuwasha moto kwenye ardhi

  Kuwasha moto kwenye ardhi na kukusanya kuni kwenye ardhi unahitaji ruhusa ya mmiliki wa ardhi . Hiyo siyo sehemu ya haki ya kila mtu. Ikiwa kuwasha moto kutafanyika kwenye sehemu zilizowekewa alama ya kuwa sehemu ya kuwasha moto, inaruhusiwa. Kwenye njia ya kutembea ya Kokkola inaruhusiwa kuwasha moto tu kwenye sehemu zilizowekewa alama kuwa sehemu ya kuwasha moto.

  • Inaruhusiwa kuwasha moto tu kwenye sehemu zilizowekewa alama.
  • Wakati wa tahadhari ya moto wa kwenye nyasi au msituni hairuhusiwi kabisa kuwasha moto.

  Piirros, jossa vaalanpunainen ja vihreäsilmäinen Kola-Kuutti grillaa nuotiopaikalla. Kola-Kuutti on Kokkolan nimikkohahmo.

 • Ikiwa pamoja na kujiandaa vizuri kwa kutembea kunatokea ajali au hali ya hatari jaribu kufanya mambo kwa utulivu na kwa kufikiri. Ujuzi wa huduma ya kwanza unasaidia, kwa hiyo inafaa kuwa na ujuzi!

  Makadirio ya hali

  • kuzuia ajali zaidi
  • huduma ya kwanza pamoja na mengine kusimamisha kutoka damu na kuhakikisha ufanyaji kazi wa njia ya kupumua na moyo, ikihitajika hatua za kuamsha
  • kuomba msaada, simu ya kituo cha dharura 112 (pamoja na gari la wagonjwa)
  • kushughulikia hali mpaka msaada wa ziada ufike

  Piga simu namba ya dharura 112, ikiwa

  • suala ni la dharura
  • suala linahusu hali ya hatari ya ukweli
  • inahitajika msaada wa dharura wa kiofisi (polisi, huduma ya kwanza, uokoaji na ofisa wa ustawi wa jamii)
  • ikiwa uhai au afya unatishiwa au uko hatarini
  • au ikiwa kuna sababu ya kushuku kuwa hivyo.

  Unapotoa taarifa eleza;

  1. unapiga simu kutoka wapi
  2. kitu gani kimetokea
  3. subiri maelekezo ya kitu cha kufanya
  4. usizime simu kabla hujapewa ruhusa.